Messages from the Word of God by Br. David Nelson, Evangelist
Available bi-monthly on cassette or CD.
All materials free as the Lord provides.
Messages from the Word of God by Br. David Nelson, Evangelist
Available bi-monthly on cassette or CD.
All materials free as the Lord provides.
Kama unanifanana, unataka kujua jinsi mtu Fulani anaamini kuhusu mafunzo
muhimu ya bibilia.Natumahi maneno haya machache yatakufahamisha kuhusu
tunaposimama kwa haya mafunzo muhimi ya ukweli ya bibilia.
i.Bibilia.
Tunaamini kwa kuambiwa na kutiwa motisha na ufunuo mpya na ule wa
kale.Bibilia inasimama hadi mwisho na haina dosari.Haina makosa yoyote.Bibilia
pekee ndiyo sheria ya kuaminika na kutenda.Tunaamini kifungu cha mfalme James
kwa wale waongeao kizungu.1 Timotheo 3:16;1 petero 1:21’Methali30:5,Zaburi
119:89,160;Mathayo 5:18,Warumi 3:1,2.
ii.Mungu.
Tunaamini mungu mmoja anayejifunua kupitia njia tatu.Baba,Mwana na roho
mtakatifu.Hawa si miungu mitatu bali ni mmoja.Wako sawa,milele na wa chanzo
moja.Lakini wako tofauti na wako na maumbile tofauti mbele za Mungu.
1.Mungu Baba.
Baba ni mtu bali si mfano wa wema.Ako na hisia,upendo,chuki,wivu na
kadhalika.Yeye si mfano bali yu afanya kazi duniani
leo.1johana1:3,Kutoka20:5,6,Nahumu 1,2,Methali 6:16-19:Danieli 2:21.
2.Mungu Mwana.
Mungu mwana alikuwa na Baba siku ya mwanzo ya kuumba dunia.Alikuja kwa hii
dunia na alijitoa sadaka kwa sababu ya dhambi za binadamu.Alifufuka katoka
kifoni na akapanda mbinguni anapokaa katika mkono wa kulia wa Baba.Atarudi
humu duniani kuchukua uzima wa dunia.Johana1:1-14:Mathayo1:18-25,Luka
1,2;Mariko 10:45Mathayo27:1,Wakoritho15,Isaia 7:14:Tito 2:13 1 Thesalonika
4:16,Ufunuo 1:7,19:11-16;wakolosai1:15-17
3.Mungu roho mtakatifu.
Roho mtakatifu ni mtu hivyo basi hafai kutajwa kama kitu.Alikuwepo wakati
wakati wa kuumba dunia.Alipatia watu nguvu katika agano kuu kuweza kufanya
kazi ya mungu.Leo anahukuma kwa dhambi,anaishi ndani yetu na analinda
waokovu na hutufungulia mambo ya mungu.
Mwanzo1:2: Matendo ya mitume5:3, 4: Warumi 88:9-16, 16:7-14.
iii.Shetani.
Tunaamini shetani ni mtu na sio mfano wa matendo maovu.Hakuumbwa muovu
bali aligeuka kuwa muovu alipojaribu kutenganeza uongozi mbinguni.Anafanya
kazi humu duniani lakini atahukumiwa aende jehanamu kuteseka milele.Mwanzo
3:1-5,14-16;job 1,2;isaia 14:12-17;Ezekieli 28:11-19;Mathayo 4:1-11;Luka4:1-
13;peter5:8 yohana 8:44 ufunuo 20:1,2,7-10
iv.Kuumba.
Tunaamini ujumbe wa siku sita zilizoandikwa kwenye kitabu cha
mwanzo1,2;wahebrania11:3;wakolosai 1:16,17
v.Binadamu.
Tunaamini binadamu aliumbwa kwa mfano wa mungu na wala hakutoka kwa enzi
za kujiendeleza.Adamu binadamu wa kwanza aliwekwa kwenye shamba la edeni
kulilinda.Alipojaribiwa na shetani binadamu alitenda dhambi.Dhambi ilileta kifo
kwa binadamu maramoja kwa roho,kuendelea kwa moyo na mwisho kwa mwili
wake.Binadamu leo anazaliwa kwenye dhambi.Hivyo basi anahukumiwa na
Mungu na hawezi kurudisha upendeleo wa mungu kwake.Mwanzo1:26-28,2:2-
25,3:1-24;Warumi 3:10,23;Wagalatia 2:16;warumi 5:12-14
vi.Wokovu
Kwa sababu ya dhambi,watu wote wanahukumiwa mbele ya mungu na wanahitaji
wokovu.Binadamu hawezi kuwa mzuri kabisa au kufanya matendo mazuri
kujipatia wokuvu.Yeye hawezi kujiokoa mwenyewe.Hivyo mungu alitengeneza
njia ya kulipa dhambi nah ii ilikuwa kupitia damu ya mwana wake.Yesu kwa kifo
chake alitimiza mapenzi ya Mungu mtakatifu.Kuegemea uzuri wa yesu,Mungu
anawaita watu wapokee wokovu.Wokovu unatokana na mapenzi ya mungu wala si
kupitia uwezo wa binadamu.Mungu anawaita binadamu watubu dhambi wapate
uaminifu wa yesu kristo.Tunaamini ulinzi wa milele wa wokovu.
Mariko 10:45;Isaiya 45:22,Yohana 3:17,18;waefeso 2:8,9;Warumi 5:15-23,Tito3:5
Wahebrania 10:45 Yohana 10:10-18
vii.Kanisa.
Tunaamina kuwa kanisa ni ya waumini wa hapa waliobatizwa na kukubaliana
pamoja na injili ana ofisi mbili ya muhubiri wasaidizi.Hao watu lazima wawe
wamefaulu kulingana na maandiko.Tunaamini kuwa wenyeji wa kanisa yako
wanastahili waishi maisha tofauti nay a dunia nay a mungu.Kanisa inaangalia
maneno mawili,ubatizo na meza iliyoandaliwa na yesu.Hayo yote yanaangaliwa
kwa agano jipya la kanisa.Tunaamini kuendelea kwa kanisa kutoka siku ya
yesu.Mathayo 16:16,19;mathayo 28:18/19;Warumi6:4,5;matendo ya mitume 1:8 1
Timotheo3:1-13;1wakoritho11:20-34;2Wakoritho6:13-18
viii.Mambo ya mwisho.
Tunaamini kurudi kwake yesu kristo kuchukua watu wake peponi.Tunaamini
kuteseka kutaikumba dunia yote.tunaamini kurudi kwa yesu duniani,tunaamini
uongozi wa yesu baada ya hapo,shetani atatupwa kwa shimo kwa muda mfupi.hapo
nguvu zote za shetani zatashindwa na mbingu mpya na dunia
zitajengwa.1Wathesalonia4:13-18 1wakoritho16:51-57,ufungua wa yohana19-
22,Zacharia 14:4;mathayo24
ix.Mataifa ya milele.
Tunaamini kwa mataifa ya milele,jehanamu mahali pa kuharibu milele,na
kuadhibiwa wasiotubu dhambi,waliokataa kujitolea kwa mungu kwa wokovu wa
dunia.mbinguni mahali pa kupumzikia milele ambapo kwa wale waliookoka kwa
rehema ya bwana watakaa naye milele.Watu wote wataenda mojawapo wa hizi
mahali kulingani na wajibu wao kwa yesu kristo Luka16:19-31;methali
15:24;Ufunuo wa yohana 20:10-15;zaburi 9:17;Mathayo 8:12,Yohana 14:1-
6,ufunuo wa yohana 21,22
© 2010 Hakuna upendo mkubwa kwa huduma